Tunu Zetu

Ubunifu

Shirika linazingatia ubunifu katika sekta zote za Ujenzi, Viwanda, Biashara na Huduma pamoja na Kilimo, Uvuvi na Ufugaji.

Ufanisi

Kwa kutumia rasimali kidogo na kupata matokeo chanya katika uzalishaji, shirika linawekeza katika ufanisi kwa watumishi wake. Shirika linazingatia ufanisi katika shughuli zake zote, muda wote.

Uadilifu

Shirika linaamini, ili mahitaji ya mteja yaweze kutekelezeka kikamifu ni muhimu mtumishi awe bora katika uzalishaji na uwajibikaji, pia hana budi kuwa mwadilifu na mwamifu katika utekelezaji wa majukumu yake. Uadilifu ndio tunu inayomfanya mtu achape kazi kwa manufaa ya shirika na kufikia malengo ya Taifa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Weledi

Katika utendaji bora wa shughuli za kiuchumi, shirika linazingatia weledi katika fani mbali mbali za kitaaluma na kiufundi. Weledi wetu ndio unalifanya shirika linafanya vizuri katika miradi inayotekelezwa kwa wateja wetu kutoka taasisi za uma na zile za binafsi.