Kampuni hii ilianzishwa mwaka 2019 ili kutoa huduma ya bima za magari, afya, ajali, nyumba, safari za majini, biashara na maisha.
Makao Makuu yake yapo Mgulani, jijini Dar es Salaam.
Lengo la kuanzishwa kwake ni kusaidia Shirika katika kuongeza mapato kwa kutumia fursa ya wateja waliopo ndani na nje ya Jeshi.
Kuanzishwa kwake kulitokana na hitaji la makampuni na miradi mbalimbali ndani ya Shirika ikiwemo miradi ya ujenzi, ulinzi
pamoja na huduma ambazo husababisha Shirika kutoa fedha kwa makampuni mengine ya huduma za bima.
Kampuni inajikita kutanua soko kwa kutafuta kazi za nje ya Jeshi hasa kwenye taasisi, makampuni, na watu binafsi ambapo kazi zinatekelezwa kwa gharama iliyopangwa na Kamishna wa Usimamizi wa Bima Nchini kwa ufanisi mkubwa.
Kuwa kampuni inayoheshimika na inayoongoza nchini katika kutoa huduma zote za uwakala wa bima.
Kuhakikisha tunatoa huduma bora za uwakala wa bima na kutumia utaalam wetu katika kujadiliana na wataalam wa masoko katika kutafuta vifurushi kwa ajili ya wateja wetu.
Utamaduni wa kuaminiana, kuwajibika na uwazi ndio thamani yetu ilipo.
Huduma za Bima za vyombo vya moto:
Kwa huduma bora ya Bima za vyombo vya moto, usisite kuwasiliana nasi kupitia njia hizi:
P.O . BOX 1964,
Dar Es Salaam, Tanzania.
Simu/WhatsApp: +255 719 078 498
email: broker@sumajkt.go.tz
au fika ofisini kwetu JKT Mgulani jijini Dar es salaam.