JITEGEMEE JKT SECONDARY SCHOOL
Jitegemee Sekondari ni shule ya wavulana na wasichana kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.
Shule hii ni ya Kutwa Pamoja na huduma ya malazi kwa wanafunzi wanaoishi mbali na shule, pamoja na wale wenye mahitaji maalumu yanayotokana na mazingira yao ya kifamilia yasiyotoa nafasi nzuri ya mwanafunzi kujisomea.
Chimbuko la shule hii ni Sera ya Elimu ya Watu Wazima ambapo mwaka 1974 ilisajiliwa kama Kituo cha Elimu ya Watu Wazima kikitoa elimu ya sekondari kwa maafisa na askari. Kwa wakati huo, Shule iliitwa Mgulani (JKT) Sekondari.
Baada ya kuwa na ongezeko kubwa la Maafisa na Askari waliopata elimu ya sekondari na mahitaji ya wazazi, Sera ya elimu ndani ya Jeshi ilibadilishwa. Kutokana na mabadiliko hayo mwaka 1985 shule ilisajiliwa kutoa elimu ya sekondari kwa wanafunzi wote.
Mnamo mwaka 2019 shule ilikabidhiwa SUMAJKT ili kuiendesha kibiashara.
Shule ilisajiliwa rasmi tarehe 01 Januari, 1985 ikiwa na namba za usajili S 0298, huku pia shule ikipata usajili wa namba ya Kituo cha Watahiniwa wa Shule (School Candidates) – S 0496 huku namba ya watahiniwa wa Kujitegemea (Private Candidates) – P 0496.
Kwa sasa shule ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 2562.
Mnamo mwaka 2019 shule ilikabidhiwa SUMAJKT ili kuiendesha kibiashara.
PROGRAMU ZA SHULE
Elimu ya Sekondari Kidato cha Kwanza hadi Kidato cha Nne (Ordinary Secondary Level – O’ Level) kwa Mikondo ya Sayansi, Biashara na Sanaa (Science, Commercial and Social Science):
- Elimu ya Sekondari kwa Wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita (Advance Secondary Level – A’ Level) kwa Tahasusi (Combinations) za PCM, PCB, CBG, PGM, EGM, ECA, HGE, HGL, HGK na HKL
- Elimu ya Sekondari kwa Miaka miwili (Qualifying Test – QT)
- Maandalizi ya Kurudia Mtihani wa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa wanafunzi ambao hawakufanya vizuri.
- Darasa maalum la Wafanyakazi (Executive Class) ambao hawakufanya vizuri katika Mtihani wa Taifa Kidato cha Nne.
- Pre Form One kwa wanafunzi wahitimu wa Darasa la Saba
- Darasa la Ujasiriamali kwa Wanafunzi wote
- Kozi mbalimbali zinazoratibiwa na VETA kama TEHAMA
IDARA ZA KIMASOMO (ACADEMIC DEPARTMENTS)
Shule ina Idara za Kimasomo kama ifuatavyo:-
- Idara ya Hesabu (Mathematics Department)
- Idara ya Fizikia (Physics Department)
- Idara ya Kemia (Chemistry Department)
- Idara ya Elimu ya Viumbe – Baolojia (Biology Department)
- Idara ya Historia (History Department)
- Idara ya Jiografia (Geography Department)
- Idara ya Uraia (Civics and General Studies Department)
- Idara za Masomo ya Lugha – Kiswahili, Kiingereza na Kifaransa (Languages Departments)
- Idara ya TEHAMA (ICT Department)
IDARA ZISIZO ZA KITAALUMA (NON ACADEMIC DEPARTMENTS)
- Idara ya Utawala
- Ofisi ya Kombania ya Sekondari Jitegemee
- Idara ya Fedha
- Idara Taaluma
- Idara ya Usajili wa Wanafunzi
- Idara ya Nidhamu
- Idara ya Ukaguzi wa Ndani wa Elimu
- Idara ya Ukaguzi wa Ndani wa Hesabu za Fedha
- Idara ya Uratibu wa Dini
- Idara ya Ratiba Kuu
- Idara ya Mazingira
- Idara ya Michezo
- Idara ya Maktaba
UDAHILI WA WANAFUNZI
- Kidato cha Kwanza
Mwanafunzi anadahiliwa baada ya kuchukua Fomu ya Maombi ya Kujiunga na Shule na Kufanya Mtihani wa Kujiunga (Entrance Examination) ambapo anatakiwa kupata Wastani wa zaidi ya 41%
2. Kidato cha Tano
Wanafunzi wa Kidato cha Tano hudahiliwa (enrolment) kwa kufuata ufaulu wao wa jumla na ufaulu katika Tahasusi. Ili mwanafunzi adahiliwe Kidato cha Tano anatakiwa kuwa na Ufaulu wa jumla wa “Credit” yaani C, B au A idadi 3 na kundelea. Aidha, inatakiwa “Credit” hizo ziwe ndani ya Tahasusi (Combination husika) na Tahasusi hairuhusiwi kuwa na Ufaulu wa “F”.
3. Nafasi za Kuhamia
Mwanafunzi anatakiwa kuchukua Fomu ya Maombi ya kuhamia kidato husika. Atafanya Mtihani wa Kuhamia, kama atafaulu zaidi ya Alama 41% na nafasi zitakuwepo atadahiliwa.
Kwa Programu zingine pata maelezo na malekezo kutoka Shuleni.
Fanya kazi nasi leo
Kwa elimu bora kwanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita kwa ajili ya mwanao, usisite kuwasiliana nasi kupitia njia hizi:
P.O . BOX 45050,
Dar Es Salaam, Tanzania.
Simu/WhatsApp: +255 767 991 333/+255 716 542 777
Hotline: +255 22 2780934
email: jitegemeehighschool@sumajkt.go.tz
au fika shuleni eneo la Mtoni Mtongani, jijini Dar es salaam.