• Suma Admin
    Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kasim Majaliwa Majaliwa amefanya ziara akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Katavi. Katika ziara hio Waziri Mkuu alifanya ziara katika Hospitali ya rufaa mkoani Katavi. Fuatilia video hii hapa kupata taarifa zaidi.
  • Suma Admin
    Tarehe 12 hadi 19 mwezi Disemba 2022 kulifanyika Maonyesho ya Kibiashara eneo la ETG Moroni ambapo maonyesho hayo yaliratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro. Katika maonyesho hayo SUMAJKT ilialikwa kwa ujumbe rasmi wa balozi na uwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed. Maonyesho hayo yalikuwa na lengo la kukuza uhusiano wa kiuchumi baina ya serikali na wananchi wa nchi hizo mbili (Tanzania na Comoro) ambapo wananchi Comoro wafurahishwa na bidhaa kutoka SUMAJKT. Wananchi wa Moroni walipata fursa ya kujionea bidhaa mbalimbali zinazozakishwa na SUMAJKT na wengi walionyesha kuridhishwa na viwango vya bidhaa hizo. Katika picha unaweza kushuhudia
  • Suma Admin
    Tarehe 16 Januari 2023, Mkuu wa tawi la utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena alizindua magari 17 kwa ajili ya kuimarisha a utendaji wenye tija na kuboresha huduma za ulinzi. Aidha aliendelea kusema kwamba SUMAJKT itaendelea kutengeneza fursa mbalimbali kupitia kampuni ya SUMAJKT na hivyo kunufaisha Watanzania kwa ujumla. Bregedia Jenerali Hassan Mabena liendelea kuwashukuru na kuwaasa taasisi mbalimbali za serikali na binafsi kuendelea kufanyakazi kwa kupitia kampuni tanzu za SUMAJKT.
  • Suma Admin
    Zoezi la uzinduzi wa kuwasha umeme limefanyika Februari 17, 2023 wilayani Kishapu, katika Kijiji cha Itilima Shule ya Msingi Isunda, mkoani Shinyanga huku vijiji vitatu vikiwashiwa pia huduma ya umeme ambavyo ni Itilima, Ikonokelo na Ipeja. Mkandarasi SUMAJKT Electric Co Ltd ambaye anatekeleza mradi wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya tatu mzunguko wa Pili wilayani Kishapu na Shinyanga, ameanzakusambaza huduma za umeme katika Vijiji, Kaya na Taasisi za Serikali. Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza wakati wa uzinduzi wa kuwasha umeme wilayani Kishapu kwa vijiji hivyo vitatu, amepongeza kasi ambayo SUMAJKT Electric Co Ltd wameanza nayo ya kusambaza
  • Suma Admin
    Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh. Innocent Bashungwa akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mh. Dunstan Kyobya tarehe 8.03.2023 amefanya ziara katika shamba la SUMAJKT MNGETA PLANTATION . Shamba hilo linasimamiwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) lililopo katika tarafa ya Mngeta kijiji cha Itongowa Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro. Akiongea baada ya kukagua shamba hilo na miundombinu yake Mhe. Bashungwa amesema shamba haya kwa muda mrefu lilikaa bila matumizi yeyote baada ya mwekezaji kusitisha shughuli za kilimo. Kwa hiyo ikampendeza Mh. Rais na Amiri Jeshi Mkuu shamba hilo likabidhiwe kwa matumizi