Ifahamu SUMAJKT…
Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) ni tawi la kiuchumi linalojishughulisha na uzalishaji mali kibiashara, ili kusaidia kupunguza gharama kwa serikali katika kuendesha JKT.
SUMAJKT lilianzishwa Julai 1, 1981 kwa sheria ya Uanzishwaji Mashirika ya Kibiashara katika taasisi za umma (Act no.23 ya mwaka 1974 iliyorekebishwa mwaka 2002).
Shirika lilianzishwa kutokana na wazo la Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alitoa wazo hilo alipotembelea kambi ya JKT, Ruvu kujionea shughuli za mafunzo, malezi ya vijana na uzalishaji mali.
Shirika linafanya kazi kupitia kampuni tanzu ishirini (20) sambamba na miradi rasmi minne (4) katika sekta zifuatazo;
- UJENZI
- VIWANDA
- KILIMO, UVUVI NA UFUGAJI
- BIASHARA NA HUDUMA
Sekta hizi zinafanya kazi katika mtindo unaowezesha Shirika kujisimamia na kuleta tija katika kukuza uchumi na kuongeza kipato kwa jeshi na serikali kwa ujumla.
Mathalani, Sekta ya Ujenzi imegawanyika katika kanda 10 za Ujenzi nchi nzima ambapo kanda hizo ni;
- Kanda ya Mashariki
- Kanda ya Kaskazini Mashariki
- Kanda ya Ziwa Mashariki
- Kanda ya Kati
- Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mashariki
- Kanda ya Kusini
- Kanda ya Kaskazini Magharibi
- Kanda ya Ziwa Magharibi
- Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi
- Kanda ya Magharibi