| | |

WANANCHI WA COMORO WAFURAHISHWA NA BIDHAA KUTOKA SUMAJKT

Tarehe 12 hadi 19 mwezi Disemba 2022 kulifanyika Maonyesho ya Kibiashara eneo la ETG Moroni ambapo maonyesho hayo yaliratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro. Katika maonyesho hayo SUMAJKT ilialikwa kwa ujumbe rasmi wa balozi na uwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed. Maonyesho hayo yalikuwa na lengo la kukuza uhusiano wa kiuchumi baina ya serikali na wananchi wa nchi hizo mbili (Tanzania na Comoro) ambapo wananchi Comoro wafurahishwa na bidhaa kutoka SUMAJKT.


Wananchi wa Moroni walipata fursa ya kujionea bidhaa mbalimbali zinazozakishwa na SUMAJKT na wengi walionyesha kuridhishwa na viwango vya bidhaa hizo. Katika picha unaweza kushuhudia wananchi na maafisa wa serikali wa Comoro walijionea viwango vya bidhaa mbalimbali zinazozakishwa na makampuni tanzu chini ya mwavuli wa SUMAJKT.


Ratiba iliweza kuwaruhusu wananchi na wafanyabiashara kutembelea maonyesho hayo na kuvuna elimu, ujuzi, bidhaa na huduma mbalimbali zilizokuwa zikipatikana kwenye viwanja vya ETG Moroni. Maonyesho yalikuwa yakianza saa 3 asubuhi mpaka saa 2 usiku kila siku kuanzia tar 12 yalipofunguliwa rasmi mpaka tar 19 yalipofungwa. Maonyesho hayo yameonyesha kuwavutia wananchi Comoro wafurahishwa na bidhaa kutoka SUMAJKT na walitamani uwepo utaratibu wa maonyesho hayo kufanyika kila mwaka.

MALENGO YA MAONYESHO:

Lengo kuu la kuanzishwa maonyesho hayo ni kutanua wigo wa kibiashara baina ya nchi hizo mbili kwa kuzitambulisha fursa zilizopo baina ya Tanzania na Comoro.


Maonyesho yalikwenda na Kaulimbiu ya “Mshakamano kwa maendeleo: Tunakuza uchumi wa nchi zetu na wananchi.”

MAENEO YENYE FURSA:

Maonyesho hayo yalijaa fursa ambapo ukiachilia biashara ya bidhaa kama viatu, vikapu, vyombo vya nyumbani, nguo n.k Pia kulikua na maeneo yaliyovuta uwekezaji kama ifuatavyo;

  1. Kilimo, Mifugo na Uvuvi; Eneo hili lilitamalaki kila aina ya fursa ukizingatia Comoro ni nchi ya Uchumi wa Wastani na yenye ardhi inayofaa kilimo cha mbogamboga na mazao ya chakula. Wananchi walishawishika kuwekeza kwenye maeneo mengine kama
    i. Kuzalisha, kusindika na kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo.
    ii. Kuongeza uzalishaji wa Kuku, Mayai na Nyama.
    iii. Uvuvi.
  1. Usafirishaji; Kama tujuavyo, Comoro ni mjumuisho wa visiwa na hivyo kudhibiti mjongeo wa watu na biashara lazima kuhakikisha sekta ya usafirishaji inaimarishwa katika maeneo yafuatayo;
    i. Uwepo wa boti za kusafirisha watu na mizigo baina ya visiwa vilivyopo Comoro (inter-island transhipment)
    ii. Uwepo wa boti za Kusafirisha watu na mizigo kati ya Tanzania na Comoro.

  1. Huduma: Katika eneo hilo maonyesho yalijikita katika kuonyesha furza zilizopo kwenye;
    i. Kuanzisha Hospitali, Maabara, Vituo vya afya, vituo vya tafiti za magonjwa ya
    binadamu.
    ii. Kuanzisha vyuo vya Ufundi Stadi.
    iii. Kuanzisha karakana za vyombo vya moto.
    iv. Kuanzisha taasisi za fedha zikiwemo Benki.
    v. Huduma za Kutuma na Kupokea fedha kati ya Tanzania na Comoro.

  1. Biashara; Eneo hili lilikua ni pana na liligusa kada mbalimbali kama;
    i. Vifaa vya Ujenzi kama simenti, mabati, mbao n.k
    ii. Fenicha za aina zote.
    iii. Dhahabu na vito vya thamani.
    iv. Bidhaa za Chakula kama mchele, unga, ngano, maharage, mbogamboga na matunda.

MATARAJIO:

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro hutumia Maonyesho ya Kibiashara na Mikutano mbalimbali katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi baina na nchi hizi mbili. Hivyo, maonyesho haya yamekuwa chachu katika kuzitambua fursa za kibiashara na uwekezaji zinazoweza kuleta tija baina ya serikali na wananchi.
Maonyesho yalifungwa rasmi tarehe 19 Disemba 2022 huku yakiwa na matarajio makubwa kufanyika wakati ujao na hivyo kuendelea kugusa maisha ya wananchi ambao walifurahishwa na bidhaa kutoka SUMAJKT na kuleta tija kwa nchi washirika.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *