Tuzo zetu

Hizi hapa ni sehemu ya tuzo ambazo SUMAJKT imeweza kutunukiwa katika utendaji wake

Tuzo ya Mshindi wa Jumla katika Maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika kitaifa mkoani Dodoma. Tuzo hii tulikabidhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.

Tuzo ya Mshindi wa Jumla katika Maonesho ya Kibiashara ya Sabasaba yaliyofanyika kitaifa mkoani Dar es Salaam.

Tuzo ya mshindi wa tatu (3) katika maonesho ya biashara ya sabasaba mwaka 2023.

Tuzo ya Mshindi wa Jumla katika Maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika kitaifa mkoani Dar es Salaam. Tuzo hii tulikabidhiwa katika kipengele cha Kilimo, Uvuvi na Mifugo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Phillip Isdory Mpango (wa pili kulia) akikabidhi tuzo ya Mshindi wa Bidhaa bora zinazotengenezwa nchini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT, Brigedia Jenerali Petro Ngata kwenye kilele cha Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) katika viwanja vya Mwalimu JK Nyerere mkoani Dar es salaam.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt Stergomena Tax (Mb) (Kulia), akimkabidhi Tuzo ya miaka 41 ya SUMAJKT Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata kwa niaba ya Luteni Kanali JS Luchunga (Mstaafu) aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT mwaka 1984 – 1995, katika kilele cha maadhimisho hayo yaliyofanyika Hoteli ya Serena, Dar es salaam. Katikati ni Mkuu wa Majeshi ya Ulizni Jenerali Jacob Mkunda.

Tuzo ya Muwasilishaji bora wa bidhaa za Kitanzania kama ilivyodhaminiwa na Benki ya Azania.

Tuzo kutoka maonyesho ya Kibiashara ya Kimataifa (sabasaba) kama Washindi wa kipengele cha Kilimo, Bidhaa za Ufugaji na Matumizi ya Kiteknolojia.

Cheti cha utambuzi kutoka maonyesho ya Kibiashara ya Kimataifa (sabasaba) kama Washindi wa kipengele cha Kilimo, Bidhaa za Ufugaji na Matumizi ya Kiteknolojia.

Cheti cha ushiriki kutoka TANTRADE, waandaaji wa Maonyesho ya Kimataifa ya Kibiashara (Sabasaba) yaliyofanyika kitaifa jijini Dar es salaam.

Kutoka Hospitali ya rufaa ya Maweni

Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Fanya kazi nasi leo

Tembelea ofisi zetu au bofya kitufe hiki kupata mawasiliano yetu..