SUMAJKT yashinda Tuzo ya Mshindi wa Jumla katika Maonesho ya Nane Nane

SUMAJKT yashinda Tuzo ya Mshindi wa Jumla katika Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane). Tuzo hio imekabidhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajab Mabele.

Meja Jenarali Mabele amesema siri ya ushindi wa JKT katika maonesho mbalimbali nchini ni dhamira ya kufanya kazi kwa bidii na kwa ubunifu mkubwa.

Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo katika sherehe za Kilele cha Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nane Nane ambayo kitaifa yameadhimisha Jijini Dodoma na Kufungwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu hassan ambapo katika Sherehe hizo JKT imeibuka Mshindi wa Jumla wa Maonesho hhayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *