Waziri Bashungwa atembelea shamba la SUMAJKT Mngeta mkoani Morogoro

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh. Innocent Bashungwa akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mh. Dunstan Kyobya tarehe 8.03.2023 amefanya ziara katika shamba la SUMAJKT MNGETA PLANTATION . Shamba hilo linasimamiwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) lililopo katika tarafa ya Mngeta kijiji cha Itongowa Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro.

Akiongea baada ya kukagua shamba hilo na miundombinu yake Mhe. Bashungwa amesema shamba haya kwa muda mrefu lilikaa bila matumizi yeyote baada ya mwekezaji kusitisha shughuli za kilimo. Kwa hiyo ikampendeza Mh. Rais na Amiri Jeshi Mkuu shamba hilo likabidhiwe kwa matumizi ya Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia tarehe 15 Oktoba 2021.
Baada ya kukabidhiwa kwa nidhamu ya jeshi letu nimeona shamba hili limezaa matunda tayari hapa jeshi la kujenga taifa linazalisha mbegu kwa ajili ya wakulima na mazao mengine kwa ajili ya chakula ili kuimarisha
usalama wa chakula nchini.


Ameongeza kwa kusema mzalisha mbegu na mkulima wote walikuwa wanasubiri mvua inyeshe, sasa mnaona baada ya kukabidhi shamba kwa jeshi la kujenga Taifa linatoa mchango mkubwa wa uzalishaji mbegu mbalimbali hasahasa mbegu za mpunga na mahindi.

“Nampongeza sana Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele kwa usimamizi mzuri wa shamba hilo lakini Jeshi la kujenga Taifa kuwepo hapa linasaidia pia katika masuala ya ulinzi.”

Kwa upande wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Nduku mabele amesema matumizi ya shamba hili yanakwenda sawasawa na mipango ya muda mrefu ya SUMAJKT vilevile yanaendana na mipango ya Taifa katika sekta ya Kilimo ukuzaji wa uchumi wa Taifa kwa Ujumla.

Waziri Bashungwa atembelea shamba la SUMAJKT Mngeta mkoani Morogoro.

SUMAJKT inatamani kuendelea kuitumia sehemu hii kama nilivyosema tangu awali shamba hili tulikabidhiwa kwa ajili ya kuliendeleza na kuhakikisha kuwa miundo mbinu yake inaendelea vizuri. Pia Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Shija Lupi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji ameshukuru kwa Ugeni huo Ukiongozwa na Mh. Waziri wa Ulinzi na JKT kufika kujionea shughuli za uzalishaji mali zinavyoendelea shambani hapo ambapo Mh. Waziri
ameahidi kutatua changamoto chache zilizopo katika shamba hilo.

Nae Meneja wa shamba la SUMAJKT Mngeta Plantation Meja Gaudance Msaka amesema kuwa, mwaka huu 2023 wamelima hekari 2000 zote wameshapanda na mpunga unaendelea vizuri kazi kubwa iliyopo kwa sasa ni utunzaji wa mazao yaliyopo shambani.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *